Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Wizara ya Fedha

Baraza la Rufani za Kodi (TRAT)

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

NDIYO, Baraza limetoa "Tanzania Tax Law Reports" 2002-2010 kwa kurahisisha rejea kwa wanasheria, washauri wa kodi, wasimamizi wa kodi, taasisi za elimu (wanazuoni) na walipa kodi kwa ujumla. Jinsi ya kupata nakala ya ripoti, wasiliana na Msajili wa Baraza.
Mtu yeyote ambaye hataridhika na maamuzi ya Baraza anaweza kukata Rufaa katika Mahakama ya Rufani ya Tanzania akipinga maamuzi ya Baraza yote ama sehemu ya maamuzi hayo kwa kadri anavyoona inafaa.
Mtu yeyote anayekata rufaa anatakiwa kulipia ada isiyorudishwa ya Tshs. 30,000 kwa ajili ya notisi ya rufaa, Tshs. 150,000 kwa ajili ya rufaa, Tshs. 40,000 kwa ajili ya maombi ya kuongeza muda wa kukata rufaa, Tshs. 20,000 kwa ajili ya maombi ya utekelezaji wa maamuzi au amri ya Baraza.
Mtu yeyote ambaye hakuridhika na maamuzi ya Bodi ya Rufani za Kodi anaweza kukata rufaa ndani ya siku thelathini toka siku mrufani alipopokea uamuzi wa Bodi na kusudio la kukata rufaa linapaswa kuwasilishwa kwa wahusika wote ndani ya siku kumi na nne (14) tangu siku ya maamuzi.
Mtu yeyote ambaye hakuridhika na maamuzi ya Bodi ya Rufani za Kodi anaweza kukata rufaa Baraza la Rufani za Kodi dhidi ya maamuzi hayo yote ama sehemu ya maamuzi hayo.
Baraza la Rufani za Kodi ni chombo chenye hadhi ya kimahakama kilichoanzishwa kwa mujibu wa sheria "Tax Revenue Appeals Act" Sura ya 408. Kazi yake kubwa ni kusikiliza na kuamua Rufani za kodi kati ya walipa kodi na Mamlaka ya Mapato itokanayo na sheria za kodi zinazosimamiwa na Mamlaka ya...